Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete amesema hafurahishwi na tabia ya vijana wengi kutumia muda mwingi kuchati kwenye simu na kuacha utamaduni wa kusoma vitabu.
Ameyasema hayo jijini Dar es Salaam kwenye kongamano la 13 lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kusherehekea miaka 100 ya kuzaliwa kwa Mwalimu Julius Nyerere.
Amesema falsafa ya Mwalimu Nyerere ya kupata maarifa kupitia vitabu na machapisho inapaswa kuenziwa, na kwamba ni bahati mbaya wananchi wameacha kusoma vitabu na kutumia muda wao mwingi kuchati na simu.
“Taifa letu liko kwenye hali bora sasa kuliko tulipotoka, kuna mengi ya kufanya kuliinua zaidi ili tufike mbali kimaendeleo na kiuchumi, ni lazima tuwainue vijana kuendeleza hilo watufikishe kwenye ile nchi ya ahadi kwa sababu bado hatujaifikia,” amesema Kikwete.