Rais Samia: Msiwabambike wananchi bili za maji

0
14

Rais Samia Suluhu Hassan amewasihi wanaotoza bili za maji kuacha tabia za kuwabambika bili wananchi ili kufidia gharama za uendeshaji za ofisi zao.

Akizungumza mkoani Kagera leo Juni 9 wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji wa Kata ya Kyaka, Wilaya ya Missenyi, Rais amesema wananchi walipe bili kulingana na matumizi yao.

“Niseme na watoto wangu wanaotoza bili za maji, msiwabambikizie wananchi bili za maji, wananchi walipe maji jinsi wanavyotumia, wasiwabambikiziwe mabili kwa gharama za uendeshaji za maofisini kwenu,” amesema Rais Samia.

Aidha, amewaagiza waziri wa maji na katibu mkuu kuwakopesha mamlaka za maji za maeneo hayo shilingi milioni 500 ili ikawe nyezo ya kuunga maji kwa wananchi kwa haraka.

Amesisitiza kuwa mamlaka zitakazokopeshwa pesa hizo zitahitajika kuzirudisha ili zipelekwe kwenye mamlaka nyingine, na wananchi wa maeneo mengine pia wapate huduma ya kuungiwa maji kwa haraka.

Mwisho amewataka wananchi wa eneo hilo kutunza miundombinu ikiwemo kuutunza Mto Kagera kwa kuwa ni tegemeo kubwa kwa wananchi wa eneo hilo katika kupata huduma ya maji na kuifanya huduma hiyo iwe endelevu.

Send this to a friend