Wanaowatumia wazee kuomba mitaani kuchukuliwa hatua

0
33

Serikali imesema itawafuatilia na kuwachukulia hatua za kisheria watu wanaowatumikisha wazee kuombaomba mitaani.

Ameyasema hayo Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Maalumu, Dkt. Dorothy Gwajima jijini Dar es Salaam kuelekea Siku ya kupinga ukatili kwa wazee duniani ambayo huadhimishwa Juni 15, kila mwaka.

Aidha, Gwajima amesema lengo la maadhimisho hayo ni kuelimisha jamii kuhusu kupinga ukatili wa aina zote dhidi ya wazee ukiwamo wa kimwili, kihisia na kiuchumi pamoja na kuielimisha jamii juu ya mila potofu dhidi ya wazee.

Ahukumiwa jela maisha kwa kumlawiti mtoto wa dada yake

Hata hivyo, ameongeza kuwa Serikali inafanya mpango wa kutengeneza makazi ya wazee kila kanda pamoja na kuwaazishia miradi.

Send this to a friend