Masauni atua Loliondo, atoa maagizo kuhusu uwekaji mipaka

0
13

Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamad Yussuf Masauni amefika katika Tarafa ya Loliondo wilaya ya Ngorongoro kuona zoezi linalo endelea la uwekaji mipaka katika Pori Tengefu la Loliondo.

Masauni ameitaka Idara ya Uhamiaji kusimamia uingiaji na utokaji wa wageni katika mipaka ya nchi kwa kufuata sheria za nchi.

Aidha, amebainisha kuwa serikali itafanya uhakiki wa kina kubaini uendeshaji wa asasi za kiraia nchini kufanya kazi zao kwa mujibu wa sheria na zile zitakazokiuka zitachukuliwa hatua kali za kisheria.

Masauni ameeleza kuridhishwa kwake na maendeleo ya zoezi na kuwataka wahusika kuhakikisha kuwa zoezi hilo linakamilika kwa wakati.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Mwalimu Raymond Mangwala aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongela, amemueleza waziri kuwa amepokea maelekezo yake na kwamba atahakikisha kuwa hali ya usalama wa wananchi na mali zao inaendelea kuimarishwa na kuwa zoezi hilo litaendelea kwa hali ya amani na utulivu.

Send this to a friend