Mwigulu: Si kila mwenye miaka 18 atalipa kodi

0
11

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema kodi haitotazwa kwa kila mtu mwenye umri wa miaka 18, bali atatozwa mtu mwenye kipato ambacho kinaangukia wigo unaotakiwa kutozwa kodi.

Waziri Mwigulu amezungumza hayo ili kuwaondoa hofu wananchi kufuatia kauli ya ulipaji kodi kwa wenye umri wa mika 18 iliyotolewa katika bajeti ya 2022/23 Juni 14 bungeni Dodoma.

“Kuhusu kodi haitozwi kila mtu, anatozwa mwenye kipato, kwa hiyo mtu mwenye kipato ndiye anayetozwa kodi sio mtu mwenye kitambulisho cha taifa. Kitambulisho cha taifa ni utambuzi lakini kodi anatozwa yule mwenye kipato, watu wasipate hofu sisi, tunawarahisishia,” amesisitiza Mwigulu Nchemba.

Aidha, amesema kuhusu namba ya utambulisho ya mlipa kodi kwa mtu ambaye anataka kuanzaisha biashara asisumbuliwe kuandikisha taarifa zake upya bali taarifa ziunganishwe kwenye kitambulisho chake cha taifa

Send this to a friend