Aliyehukumiwa miaka 25 jela asema hawezi kazi ngumu, aomba kupunguziwa adhabu
Ezel Kasenegala ameiomba Mahakama kumpungizia adhabu ya kifungo cha miaka 25 jela baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kukutwa na ngozi mbili za chui zenye thamani ya TZS milioni 16.37.
Kasenegela ambaye amehukumiqa adhabu hiyo au faini TZS milioni 163.670 ameiomba mahakama kumpunguzia adhabu kwani ni kosa lake la kwanza na pia amefanyiwa upasuaji hivyo hawezi kufanya kazi ngumu.
Aidha, sababu nyingine aliyotoa apunguziqe adhabu ni kuwa ana familia kubwa yenye watoto sita na wote wanamtegemea.
Hakimu Mkazi Mkuu, Said Ally Mkasiwa amesema mtuhumiwa huyo ambaye ni mkulima na mkazi wa Lulanzi wilaya ya Kilolo alikamatwa Mei 12, 2020 akiwa anaumza Ngozi hizo kwa TZS laki 5 kwa kila moja.
“Wasamaria wema walilitaarifu Jeshi la Polisi ndipo wakaweka mtego wa kumkamata wakijifanya ni wanunuzi wa ngozi hizo za chui,” amesema.