Fahamu magonjwa 6 yanayosababishwa na matumizi ya chumvi nyingi

0
46

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), mtu mzima anatakiwa kutumia kiwango cha chumvi kisichozidi gramu tano kwa siku ili kupunguza shinikizo la damu na hatari ya kupata magonjwa ya moyo.

Ulaji mwingi wa sodiamu umehusishwa na matatizo ya afya kama vile ugonjwa wa mifupa, ugonjwa wa figo au shinikizo la damu ambayo inaweza kusababisha ugonjwa wa moyo na kiharusi.

Wataalam wa afya waneaeleza kuwa, kuongeza chumvi kupita kiasi kwenye chakula kunaweza kusababisha kuzorota kwa rangi ya ngozi pamoja na ukuaji wa mtoto wa jicho.

Chama cha Moyo cha Marekani (AHA) kinasema kunapokuwa na sodiamu nyingi kwenye damu, huvuta maji zaidi kwenye mkondo wa damu. Kiasi cha damu kinapoongezeka, moyo hulazimika kufanya kazi zaidi ili kuisukuma damu kuzunguka mwilini. Hii inaweza kunyoosha kuta za mishipa ya damu na kuifanya iwe rahisi kuharibika.

Madhara ya kuvaa miwani ya urembo

AHA imeshauri watoto wachanga chini ya mwaka mmoja hawapaswi kupewa chumvi kwa sababu figo zao hazijapevuka.

Send this to a friend