Usaili wa ajira utumishi wa umma kufanyika kila mkoa

0
12

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Jenista Mhagama ameaiagiza sekretarieti ya ajira kuhakikisha mfumo wa usaili wa ajira unakwenda mikoa yote nchini.

Akizungumza leo bungeni jijini Dodoma Jenista amesema makundi mengi ya vijana hufunga safari mpaka Dodoma kwa ajili ya kufanya usaili wa ajira ambapo wanaweza kufanya usaili huo wakiwa mikoani mwao.

“Makundi ya vijana yanasafiri kutoka mikoa mbalimbali kila mara, wanakusanyika hapa Dodoma kwa ajili ya kufanya usaili, tumesikia kilio hicho. Tumefanya maamuzi, mara baada ya bajeti hii kupita, nawaagiza sekretarieti ya ajira kutekeleza maagizo ya Serikali na Mhe. Rais kuhakikisha mfumo wa usaili sasa unakwenda katika mikoa yote nchini,” amesema.

Serikali yawaombea ajira vijana wa Tanzania nchini Qatar

Aidha, Mhagama amesema kuna haja ya kwepo kwa ‘database’ (kanzidata) ili kuondoa usumbufu  kutokana na kuwepo kwa wingi wa ufaulu wa vijana wa kitanzania lakini nafasi zinakuwa chache katika sekretarieti ya ajira.

Amesema kupitia kanzidata hiyo, waliofanya vizuri lakini wakakosa nafasi, watazingatiwa kwanza panapotokea nafasi mpya.

Send this to a friend