Wanawake washauriwa kwenda na waume zao kwa Sangoma kutibiwa

0
26

Ripoti iliyotolewa na Wanamtandao wa Mkoa wa Kusini Unguja imesema Waganga wa Kienyeji wamechangia kuongezeka kwa vitendo vya udhalilishaji kwa wanawake wanaokwenda kufuata tiba kwao.

Hayo yamebainishwa wakati wakiwasilisha ripoti ya vitendo vya udhalilishaji kwa wanamtandao wa kupinga matukio hayo katika Mikoa mitatu ya Unguja iliyofanyika katika ukumbi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania [TAMWA Zanzibar], huko Tunguu wilaya ya Kati Unguja.

Wajawazito watozwa gharama tofauti za kujifungua kulingana na jinsia ya mtoto

Mjumbe wa mtandao huo, Sabaha Ali Hassan amesema wanawake wengi hupatwa na majanga hayo kutokana na aina ya tiba wanazopewa na waganga wakiamini kumalizika kwa matatizo yao lakini hali inapokuwa tofauti ndipo hutoa siri ya kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji.

“Tunafahamu kwamba mtu anapokwenda katika kutafuta dawa hufanya siri lakini sasa hivi dunia imeharibika, hivyo ni vyema kwenda na mwenzako unaemuamini ili kujiepusha kufanyiwa vitendo hivyo,” amesema

Send this to a friend