Imeelezwa kuwa wanawake huishi umri mrefu zaidi kuliko wanaume. Mwaka 2018, wastani wa umri wa kuishi ulikuwa miaka 76.2 kwa wanaume na miaka 81.2 kwa wanawake.
Umewahi kujiuliza kwanini? Hizi ni sababu za wanaume kufariki haraka kuliko wanawake.
Kufanya kazi hatari zaidi.
Wanaume ni wengi zaidi kuliko wanawaka na huwaweka kwenye hatari ya kufariki mara 10 zaidi kuliko wanawake, ikiwa ni pamoja na mapigano ya kijeshi, kuzima moto, na kufanya kazi katika maeneo ya ujenzi, matengenezo na ukarabati.
Vifo kwa magonjwa ya moyo
Wanaume wana uwezekano wa asilimia 50 zaidi wa kufariki kwa ugonjwa wa moyo kuliko wanawake.
Ukweli ni kwamba wanaume wana viwango vya chini vya estrojeni kuliko wanawake hii inaweza kuwa sehemu ya sababu. Lakini hatari za kiafya, kama vile shinikizo la damu, dhidi au viwango vya cholesterol visivyofaa, vinaweza pia kuchangia.
Kujiua
Maswala ya afya ya akili yanaendelea kuathiri idadi ya wanaume kwa njia isiyo sawa. Wanaume hufa kwa kujiua mara tatu zaidi kuliko wanawake kutokana na sonona inayopelekea kuchukua hatua mbaya zaidi.
Sababu ya kujiua hutokana na hali ngumu ya maisha, mahusiano, kufukuzwa kazi, na kadhalika.
Kutokwenda Hospitali
Kulingana na Shirika la Utafiti na Ubora wa Huduma ya Afya, wanaume wana uwezekano mkubwa wa kupuuzia kwenda hospitali kwa ajili ya kupata matibabu au kufanya ziara za kawaida za hospitali kwa ajili ya uchunguzi wa afya kutokana na kujijengea kutojali maumivu yoyote ya kimwili na kihisia.
Lishe duni na Mazoezi.
Lishe yenye virutubishi vingi na mazoezi ya kawaida ni muhimu ili kudumisha afya bora. Zote mbili zimethibitishwa kupunguza hatari ya magonjwa sugu, kama vile ugonjwa wa moyo, shinikizo la damu na kisukari.
Walakini, wanaume wana uwezekano mdogo wa asilimia 50 kuliko wanawake kudumisha lishe bora yenye matunda na mboga.