Kifungu cha 77 cha Sheria ya Usalama Barabarani kinamtaka kila mwendesha chombo cha moto kutembea na leseni barabarani, na pia trafiki ana mamlaka ya kumsimamisha na kumtaka aoneshe leseni kila mwendesha chombo cha moto.
Lakini, si kweli kuwa mwendesha chombo cha moto asipoonesha leseni kwa wakati huo tayari ametenda kosa.
Kifungu cha 77[1] cha Sheria ya Usalama Barabarani kinasema kuwa, mtu hatatiwa hatiani, kwa maana ya kulipa faini, kuandikiwa kosa au kuadhibiwa na mahakama kwa kosa la kutoonesha leseni pale anapoombwa.
Bei mpya za mafuta kwa mikoa yote kuanzia Julai 6, 2022
Mtu anaposimamishwa na akaombwa kuonesha leseni ila akawa hana kwa wakati huo, sheria inasema mtu huyo anazo siku tatu ili kupeleka na kuonesha sehemu husika.
Anachotakiwa kufanya askari si kuandika kosa, bali kukutaka uoneshe leseni hiyo ndani ya siku tatu tangu siku hiyo, na mara mtu atakaposhindwa kuonesha ndani ya siku hizo, ndipo linaweza kuwa kosa.