Waziri wa Nishati, Januari Makamba ameanza ziara ya siku siku 21 katika wilaya 38 za mikoa 14 kuhamasisha matumizi ya nishati salama ya kupikia inayoanza leo.
Akizungumzia ziara hiyo iliyoanza leo ikilenga kunusuru maisha ya Watanzania hasa wa vijijini ambao wanatumia zaidi kuni amesema wizara yake imeamua kuipa kipaumbele suala la nishati ya kupikia kwa kuwa ni tatizo linalogharimu maisha ya Watanzania.
Ameeleza kuwa zaidi ya Watanzania 22,000 wanapoteza maisha kila mwaka kutokana na magonjwa ya upumuaji yanayosababishwa na matumizi ya nishati isiyo salama ya kupikia.
Watu 19 wauawa nchini Afrika Kusini
“Tutaenda kuhamasisha matumizi ya nishati safi na salama, kwa kuelimisha wananchi kutumia nyenzo salama za nishati kwa ajili ya matumizi ya kupikia,” amesema Makamba.
Aidha, Makamba amesema katika ziara hiyo itaahamasisha na kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini ili kuhakikisha inatekelezwa kwa kasi na kwa kiwango cha ubora kinachotakiwa.
Pia, jambo lingine ambalo litafanyika kwenye ziara hiyo ni kusimamia upatikanaji wa mafuta safi vijijini kwa kuhakikisha vituo vya mafuta vinajengwa ili kuwahikikishia wakazi wa vijijini wanapata mafuta safi.
Ziara hiyo itafanyika katika mikoa ya Mara, Mwanza, Kagera, Geita, Katavi, Tabora, Shinyanga, Songwe, Simiyu, Rukwa, Mbeya, Njombe, Ruvuma na Mtwara.