Benki ya Dunia: Tanzania inaweza kuwa ghala la chakula

0
28

Benki ya Dunia imeipongeza Tanzania kwa kuwekeza kiasi kikubwa cha fedha kwenye maeneo ya uzalishaji ikiwemo kilimo, mifugo na uvuvi mambo ambayo yatachochea ukuaji wa kipato cha wananchi na kukuza uchumi wa nchi.

Hayo yametolewa Jijini Dar es Salaam na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Kusini Mashariki, Victoria Kwakwa alipokutana na kufanya mazungumzo rasmi na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba.

Kwakwa ameahidi kuwa benki na washirika wake watasaidia juhudi za Serikali za kufanikisha mapinduzi katika sekta hizo muhimu kwa kutoa fedha pamoja na ushauri wa kitaalamu ili mpango huo wa kuendeleza kilimo, mifugo na uvuvi uwe na tija.

Amesema changamoto ya UVIKO 19 na vita vinavyoendelea baina ya Urusi na Ukraine vimeibua changamoto kubwa ya uhaba wa mazao ya nafaka, na kwamba Tanzania ikijipanga vizuri inaweza kuwa ghala la chakula na kuifanya ijitosheleze kwa chakula bila kuagiza kutoka nje.

Watu 19 wauawa nchini Afrika Kusini

Kwa upande wake Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba ameishukuru Benki hiyo kwa kuiidhinishia Tanzania kiasi cha TZS Trilioni 4.9 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kupitia mpango mpya wa utoaji mikopo na misaada wa IDA 20 ulioanza kutekelezwa rasmi mwezi Julai, 2022.

Send this to a friend