Vigogo 39 wadaiwa kukwapua eneo la wananchi Mwanza, waziri aingilia kati

0
24

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula ameagiza wizara kufanya uchunguzi juu ya madai ya vigogo 39 waliomilikishwa eneo bila kufuata utaratibu.

Agizo hilo limekuja baada madai ya kuchukuliwa kwa eneo la makazi la Isamilo jijini Mwanza lenye viwanja 39, linalolalamikiwa na wananchi wakidai eneo hilo lilichukuliwa bila wao kulipwa fidia yoyote na kuuzwa kwa watumishi wa Serikali licha ya wao pia kujaza fomu za ununuzi wa eneo hilo.

Mabula amewataka wananchi kutoa ushahidi wa viwanja ambavyo wanadai watumishi wamejimilikisha ili kuchukua hatua endapo itabainika ni kweli wamekwenda kinyume na taratibu.

“Kama ni mtumishi leteni taarifa zao tutashughulikia, Serikali ya Mama Samia Suluhu Hassan haipo katika kulea maovu, ipo katika kuhakikisha kila mmoja anapata haki yake,” amesema.

Juni 2 mwaka huu, Jiji la Mwanza lilitangaza kuuza viwanja katika eneo la Isamilo na kila mwombaji alitakiwa kulipia TZS 20,000 kwa ajili ya fomu ambapo baadhi ya wananchi wamedai kulipia lakini hawakuwahi kupata majibu

Send this to a friend