Mrema asema katiba mpya siyo mwarobaini wa matatizo nchini

0
34

Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP), Augustino Mrema amesema wananchi hawapaswi kuaminishwa kwamba katiba mpya ndiyo tiba ya kutatua kila tatizo lilipo nchini.

Ameyasema hayo baada ya kuwasilisha maoni yake mbele ya kikosi kazi maalum kilichoundwa kukusanya maoni mbalimbali kuhusu demokrasia, na kusisitiza kuwa jambo muhimu kwa sasa ni kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan katika juhudi za maendeleo.

Mrema ameeleza kwamba kwa sasa jambo hilo halina umuhimu kwa kuwa zipo baadhi ya nchi zilizoipa kipaumbele suala la katiba na limeshindwa kuwasaidia.

Utafiti: Wanaowahudumia wenye magonjwa yasiyoambukiza hatarini kupata magonjwa hayo

“Zipo nchi kama Kenya na Marekani ambazo pamoja na kufanya mabadiliko ya katiba zao hazijaweza kuwasaidia. Mfano mzuri ni Marekani ambayo licha ya kufanya mabadiliko katika katiba yake, bado Rais aliyepita (Trump) alilalamika kuibiwa kura,” amesema.

Aidha, Mrema ametoa ushauri kwa Serikali kuwa kutokana  na umuhimu wa Tume Huru ya Uchaguzi, kuna haja ya kuundwa kwa chombo kitakachotoa usaidizi wa suala hilo ili kutoa haki na kutatua changamoto zinazojitokeza wakati wa uchaguzi.

Send this to a friend