Serikali yakabidhi tozo ya maegesho ya magari Manispaa

0
18

Serikali imekabidhi kazi ya tozo ya maegesho ya magari (packing) katika manispaa za jiji la Dar es Salaam kutoka kwa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA).

Akizungumza na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mkuu wa Mkoa, Amos Makalla amesema lengo la kuikabidhi manispaa ni kuondoa kero zinazosababishwa na mifumo iliyowekwa katika ukusanyaji.

Makalla amesema lengo lingine  ni kuondosha vishoka wanaokusanya tozo za maegesho kiholela ambao hawajasajiliwa na  kampuni yeyote.

Mambo matatu ya kufanya unapozimikiwa na gari njiani

Aidha, amesema watu wote watakaopewa  kazi hiyo  wawe na vitambulisho ili waweze kutambulika na jamii kwa lengo la kuzuia utapeli unaofanywa na baadhi ya watu wasiohusika.

“Vaa kitambulisho, onesha mahali ambapo sitakiwi kupaki, lugha nzuri, mtu mwenyewe afanye kosa unajua huyu kafanya kosa mwenyewe. Sijawaambia msikusanye, kusanyeni kwa mujibu wa sheria lakini tutengeneze mazingira mazuri ya ufanyaji kazi kwa ufanisi bila kuleta kero kwa wananchi,” amesema.

Mbali na hayo, Makalla amezisihi kampuni zinazorasimisha ardhi kujiepusha kuwa sehemu ya matatizo ya ardhi katika maeneo yenye migogoro.