Polisi wakamata mifugo 1,448 iliyoharibu ekari 387 Kilimanjaro

0
27

Jeshi la Polisi kupitia Kikosi cha Kuzuia Wizi wa Mifugo na Migogoro ya Mifugo Tanzania limekamata mifungo 1,448 ambayo imeharibu jumla ya ekari 387 ya mashamba ya wakulima yenye mazao tofauti tofauti yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 660.

Kamanda wa kikosi hicho, Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP. Simon Pasua amethibitisha kukamatwa kwa mifugo hiyo mnamo Julai 9, 2022, maeneo ya Kijiji cha Olmolog katika Halmashauri ya Wilaya Siha mkoa wa Kilimanjaro.

Kamanda Pasua ameitaja mifugo hiyo kuwa ni Ng’ombe 485, Mbuzi na Kondoo 963, na kwamba uchunguzi wa awali umebaini kuwa mifugo hiyo imetoka nje ya mkoa wa Kilimanjaro na kuingia katika wilaya ya Siha bila ya kufuata utaratibu.

Aidha, amesema baada ya kukamatwa kwa mifugo hiyo, hakuonekana mmiliki wao mpaka taratibu za kimahakama zilipokamilika na umuazi kutolewa juu ya uharibifu wa mazao hayo, ambapo Mahakama ya Wilaya Siha iliamua mifugo hiyo itaifishwe.

Hata hivyo, ametoa wito kwa wafugaji kuepuka migogoro baina yao na wakulima, na badala yake amewaomba kufuata maeneo yaliyotengwa kwaajili kwa kulisha mifugo yao na kuepusha migogoro baina yao na wafungaji.

Send this to a friend