Chuo Kikuu chapiga marufuku mavazi meusi

0
15

Uongozi wa Chuo Kikuu cha Covenant (CU) nchini Nigeria, umepiga marufuku uvaaji wa nguo zote nyeusi na viatu vya ‘Brogues’ kwa wanafunzi chuoni hapo kuanzia kipindi kijacho cha masomo.

Taasisi hiyo ya kidini inayomilikiwa na Kanisa la Living Faith Worldwide, imesema nguo nyeusi inaweza tu kuvaliwa na rangi nyingine na kusisitiza kuwa mwanafunzi yeyote atakayekiuka maagizo hayo ataadhibiwa.

“Wanafunzi wote wanapaswa kutambua kwamba kuanzia mwaka mpya wa masomo, kuvaa shati jeusi na suruali nyeusi au sketi ni marufuku, mavazi yenye rangi nyeusi yanaweza kuvaliwa na rangi zingine. Pia viatu vinavyoitwa Brogues vimepigwa marufuku,” imeandika CU kupitia tovuti yake.

Jambo hilo limezua gumzo kwenye mitandao ya kijamii huku wanafunzi wengi wakionekana kutofurahishwa na agizo hilo.