Mambo makubwa matatu ambayo IGP Wambura ataanza nayo
Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Camillus Wambura ametaja mambo matatu ambayo atakwenda kuyasimamia na kuyafanyia utekelezaji ili kuleta tija katika Jeshi la Polisi.
IGP Wambura ametaja jambo la kwanza kuwa ni kuhakikisha mapambano dhidi ya uhalifu yanadumishwa kwa kuongeza nguvu kubwa na ya kisasa katika kupambana na uhalifu ili kuhakikisha wananchi wanakuwa salama bila kuingiliwa.
Maagizo ya Makamu wa Rais kwa Balozi wa Tanzania- Indonesia
Mkakati wa pili ni kushughulikia maadili ndani ya Jeshi la Polisi. IGP Wambura ameeleza kuwa nchi haiwezi kuwa na Jeshi imara, la kisasa na lenye weledi kama hakuna maadili na nidhamu ndani ya jeshi.
Jambo lingine lililotajwa na IGP Wambura ni kuhusu haki kwa wananchi ambayo inajumuisha haki katika kila eneo, kuanzia vituo vya polisi pamoja na mitaani.
“Nataka kuona watu wanatendewa haki kwa mujibu wa sheria, lakini kwa mujibu wa taratibu. Hizi ni baadhi ya mikakati ambayo nitahakikisha inafanyiwa utekelezaji na inasimamiwa ili kuleta tija,” amesema IGP Wambura.