Dkt. Mpango akemea tabia ya kutoza ushuru mazao chini ya tani moja
Makamu wa Rais wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango amewataka wakurugenzi kuacha mara moja tabia ya kutoza ushuru kwa mazao yanayosafirishwa chini ya tani moja, kwani Serikali iliondoa tozo hizo ili kuwasaidia wakulima wadogo kupata kipato.
Amesema hayo baada ya kutembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa njia kuu ya kusafirisha umeme wa msongo wa Kilovoti 132 kutoka Tabora hadi Katavi eneo la Inyonga wilaya ya Mlele, ambapo amewaagiza wakurugenzi kutafuta mbinu sahihi za kuwabaini wanaokusanya mazao zaidi ya tani moja ili kuwanusuru wakulima wadogo.
Kenya yamzuia Rostam Aziz kujenga kiwanda cha gesi
Mbali na hayo, ameiagiza Wizara ya Nishati kuhakikisha ujenzi wa kituo cha kupoozea umeme wa gridi ya Taifa cha Inyonga kinakamilika ifikapo Oktoba 2023 na mkoa wa Katavi unaunganishwe katika gridi ya Taifa.
Dkt. Mpango yupo ziarani mkoani Katavi ambapo anakagua miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kuzungumza na wananchi.