Ummy: Hakuna mgonjwa mpya Homa ya Mgunda

0
15

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema toka Julai 18, 2022 hadi asubuhi ya leo, hakuna mgonjwa mpya aliyeonesha dalili za kuwa na ugonjwa wa Homa ya Mgunda na tayari wagonjwa wote waliokuwa wamelazwa tayari wameruhusiwa kuendelea na shughuli zao.

Akiongea na waandishi wa habari leo Dar es salaam, amewasisitiza wananchi kutokuwa na hofu kwa kuwa ugonjwa huo umedhibitiwa, na kwamba Serikali ina uwezo wa kuendelea kuchunguza, kutibu na imeweka mikakati ya kuudhibiti ugonjwa huo nchini.

Aidha, Wizara ya Afya imeendelea kuwakumbusha wananchi kuendelea kuchukua tahadhari stahiki za kujikinga na ugonjwa huo ikiwemo kuepuka kutumia maji au vitu vilivyochafuliwa na mkojo wa wanyama, kunywa maji safi na salama pamoja na wagonjwa wanaohisi dalili zilizotajwa na Wizara kufika hospitali kwaajili ya uchunguzi.