Daktari Jean de Dieu Maniriho kutoka Musanze nchini Rwanda, amehukumiwa kifungo cha miaka 25 jela baada ya kukutwa na hatia ya kumnajisi msichana wa miaka 17.
Uamuzi huo ulitolewa na Mahakama ya kati ya Musanze Julai 28 mwaka huu baada ya kesi hiyo kuchukua takribani miaka miwili.
Inadaiwa kuwa, Daktari huyo alimnajisi na kumpa ujauzito msichana wa shule mwenye umri wa miaka 17 mkazi wa Musanze, na baadaye alijaribu kuitoa mimba hivyo kusababisha msichana huyo kupoteza maisha.
Benki Kuu kuchunguza sarafu ya kughushi ya TZS 500 inayosambaa mitaani
Hata hivyo, jaji alisema katika upande wa mashtaka haukuweza kutoa ushahidi wa kutosha kumtia hatiani kwa kosa la kumuua msichana huyo.
Katika uchunguzi uliofanywa inadaiwa kuwa, Maniriho ambaye alifanya kazi kama daktari wa meno katika zahanati ya Mpore iliyoko Musanze mjini, alikiri shtaka la kunajisi na kumtoa msichana mimba lakini kesi yake ilipoanza alikana mashtaka yake yote.
Ushahidi wa kimahakama unaeleza kwamba msichana huyo alitoweka Novemba 2020 siku chache kabla ya maiti yake kupatikana katika shamba na kisha kuzikwa, lakini familia iliomba mwili ufukuliwe kwa ajili ya uchunguzi, na mara baada ya vipimo vya DNA iligundulika msichana huyo alifungwa miguu na mikono kwa kamba ya plastiki ambayo kamba hiyo ilipatikana nyumbani kwa mtuhumiwa.