Halmashauri zafikia malengo ya asilimia 100 ukusanyaji wa mapato baada ya miaka 10

0
21

Waziri wa TAMISEMI, Innocent Bashungwa ametoa taarifa ya Ukusanyaji wa mapato ya ndani na matumizi ya halmashauri kwa kipindi cha robo ya nne ya mwaka wa fedha 2021/22.

Katika taarifa yake ameeleza kuwa katika mwaka wa fedha 2021/22, halmashauri zilipanga kukusanya shilingi bilioni 863.9 kutoka kwenye vyanzo vya mapato ya ndani, huku katika kipindi cha mwezi Julai hadi Juni 2022, halmashauri zimekusanya shilingi bilioni 888.7 ambayo ni asilimia 103 ya makisio ya mwaka husika.

“Uchambuzi wa taarifa za mapato ya ndani ya halmashauri katika mwaka wa fedha 2021/22, unaonesha kuwepo kwa ongezeko la mapato halisi yaliyokusanywa kwa kiasi cha shilingi bilioni 131.7, ikilinganishwa na kiasi halisi kilichokusanywa katika mwaka wa fedha 2020/21, cha shilingi bilioni 757.1, sawa na ongezeko la asilimia 17,” ameeleza Waziri Bashungwa.

Serikali yashauri wananchi kuongeza ulaji wa nyama na mayai

Waziri Bashungwa amesema halmashauri ya Wilaya ya Kibaha inaongoza katika halmashauri zote kwa kukusanya asilimia 247 ya makisio yake ya mwaka ikifuatiwa na halmashauri za Wilaya ya Mlele asilimia 185, pamoja na halmashauri ya Wilaya ya Morogoro kwa asilimia 158.

Hata hivyo amesema kiwango hicho cha makusanyo hakijawahi kufikiwa kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita, kwani halmashauri hazijawahi kufikia malengo yao ya mwaka kwa asilimia 100.

Send this to a friend