Mambo 5 ya kuzingatia kabla ya kununua gari

0
31

Unapofikia uamuzi wa kununua gari, kuna mambo ya msingi unayotakiwa kuzingatia ili hata unapotaka kuliuza gari lako na kununua gari jingine au kununua toleo jipya, iwe rahisi kupata mteja.

Haya ni baadhi ya makosa yanayopuuzwa mwanzoni wakati wa kununua gari na mwishoni humgharimu muuzaji.

Gharama za matengenezo ya gari
Hizi ni pamoja na gharama za mafuta ya gari. Gharama za matengenezo ya gari hupanda mwaka hadi mwaka kutokana na huduma mbalimbali zinazohitajika kufanyika kwenye gari hilo, kwani kadri siku zinavyokwenda ndivyo matengenezo ya gari yanakuwa makubwa.

Epuka toleo jipya
Hushauriwi sana kununua toleo jipya la gari, kwani baadhi ya matoleo hutengenezwa na kuyapa muda wa majaribio ili kufanya maboresho katika toleo lijalo, hivyo unashauriwa kununua magari yaliyotoka miaka mitatu iliyopita.

Muda wa kununua
Sio kila mwezi ni wa kununua magari, inashauriwa miezi mizuri ya kununua magari ni kuanzia mwezi wa 12 mpaka mwezi wa tatu, kwani kampuni nyingi hutoa ofa ya kushusha bei ili kuuza bidhaa zao.

Hizi ni faida 5 za kula bamia

Jina la gari
Hapa kikubwa kinachoangaliwa ni jina la gari, kuna magari magumu sana kuingia sokoni na kununulika, kutokana na upatikanaji wa vifaa vya ziada pindi gari hilo linapoharibika. Pia inashauriwa kuzingatia rangi ya gari ambapo watu wengi hupendelea rangi nyeusi, nyeupe na rangi ya fedha.

Fanya utafiti
Usiwe na haraka ya kununua gari, fanya utafiti sehemu mbalimbali, tumia vyanzo mbalimbali vya mitandao ya kijamii, washirikishe watu wanaojua magari wakushauri juu ya gari unalotaka kununua, kusanya taarifa sahihi kisha ufanye maamuzi.

Send this to a friend