TCRA yaipa adhabu Ayo TV

0
53

Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeitaka televisheni ya mtandaoni ya Millard Ayo (Ayo TV) kuomba radhi kwa siku tatu mfululizo, kutokana na kutenda kosa la kuonesha miili ya watoto wa Shule ya Msingi ya King David, waliofariki dunia katika ajali ya gari mkoani Mtwara hivi karibuni.

Kamati imeeleza kuwa picha walizochapisha ziliudhi, kuhuzunisha na kudhalilisha marehemu.

Aidha, imesema utetezi uliotolewa na Ayo TV ulikuwa ni hafifu na hivyo imeiagiza kuzingatia utu, kanuni, misingi, sheria na viwango katika uchapishaji na uandaaji wa habarie.

Watoto nane walifariki katika ajali ya gari iliyotokea Julai 26, 2022 eneo la Mjimwema, Kata ya Mikindani, Mtwara Mjini baada ya gari walilokuwa wamepanda kupata hitilafu kwenye mfumo wa breki na kuingia korongoni.

Send this to a friend