Agizo la Dkt. Mpango kwa Jeshi la Polisi

0
13

Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango amelitaka jeshi la Polisi kutenda haki pasipo kuonea mtu yeyote, na kwamba yeyote anayevunja sheria achukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria na sio vinginevyo.

Ameyasema hayo leo Agosti 18 alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali Camillus Wambura katika ofisi ya Makamu wa Rais jijini Dar es Salaam.

Serikali yahamasisha vijana kunywa pombe

Katika mazungumzo hayo, Makamu wa Rais amelipongeza jeshi la polisi kwa kuendelea kuimarisha amani pamoja na ulinzi wa wananchi na mali zao, akisisitiza jeshi kuendelea kuhakikisha utulivu unapatikana wakati wote.

Aidha, Makamu wa Rais amemuagiza IGP Wambura kuangazia malalamiko yanayotolewa na wananchi kwa jeshi la polisi, na kuwachukulia hatua askari wachache wanaoharibu taswira ya jeshi hilo.

Send this to a friend