Ujenzi wa mwendokasi Mbagala-Gerezani wafikia 66%

0
56

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, amesema ujenzi wa mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (BRT II), awamu ya pili kutoka Mbagala hadi Gerezani umefikia asilimia 66.6 na unatarajiwa kukamilika Februari 2023.

Prof. Mbarawa amesema hayo jijini Dar es Salaam mara baada ya kukagua ujenzi wa mradi huo ambapo amefafanua kuwa kazi zinaenda vizuri huku ikitarajiwa kuwa mradi huo kukamilika kwa muda uliopangwa ili uweze kupunguza msongamano wa magari na kurahisisha usafiri.

Bolt kusitisha huduma ya usafiri kwa wateja binafsi

Aidha, amemtaka mkandarasi wa mradi huo kuhakikisha anakamilisha upande wa pili wa barabara za juu (flyover) ya Chang’ombe na Kurasini ifikapo Oktoba ili kuruhusu magari kupita juu pamoja na kukamilisha ujenzi wa daraja lenye urefu wa mita 80 eneo la BP ifikapo Desemba 2022.

Pamoja na hayo, amewataka wananchi waliopo karibu na mradi huo kutoa ushirikiano kwa mkandarasi ili mradi huo umalizike mapema iwezekanavyo.