Kocha Mkuu wa Simba, Zoran Maki amewapongeza wachezaji wa Simba SC kwa ushindi dhidi ya Geita Gold FC licha ya kuwa hawakuwa sawa kisaikolojia baada ya kufungwa katika mechi dhidi ya Yanga SC.
Ameyasema hayo katika mahojiano na Mwananchi baada ya mechi dhidi ya Geita Gold FC katika mchezo wa ligi uliochezwa katika Uwanja wa Benjamini Mkapa na kuibuka na ushindi wa mabao 3-0.
“Mechi ilikuwa ngumu sana hasa kwa upande wa kisaikolojia baada ya kufungwa na Yanga, tulitengeneza nafasi katika kipindi cha pili na kupata mabao mawili, si rahisi hasa kuwa na wachezaji wengi wapya lakini tunaimarika,”amesema.
Simba,Yanga kumiliki viwanja vyao ndani ya miezi sita
Aidha, amesema bado hajapata muunganiko mzuri kati ya wachezaji wapya na wale wa zamani kwa sababu wachezaji wengi ni wapya lakini wanaendelea kufanyia kazi kwa kila mmoja katika timu hiyo.
Zoran amesema, safu yake ya viungo washambuliaji iko vizuri kwa uwezo uliooneshwa na nyota wake wote akiwemo Okrah na Peter Banda.