Matibabu ya fistula kutolewa katika hospitali zote za mikoa

0
30

 Matibabu ya fistula kutolewa katika hospitali za mikoa
 Serikali imeweka mkakati wa kuboresha huduma ya Mama na Mtoto.

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema matibabu ya ugonjwa wa Fistula kwa sasa yanapatikana katika hospital zote za mikoa nchini ambapo awali matibabu hayo yalikuwa yakipatika katika hospitali ya CCBRT pekee.

Waziri Ummy amebainisha kuwa Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, imeweka mkakati wa kuboresha huduma za afya ya mama na mtoto pamoja na huduma za uzazi kwa ujumla.

“Hapa kazi kubwa alofanya Rais Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha ameboresha huduma za akina mama wajawazito kwa kuhakikisha wanawake wanaopata uzazi pingamizi wanapata huduma za upasuaji katika vituo vya kutolea huduma za afya na hospitalini,” amesema.

Wanawake waongoza kuugua maradhi ya moyo

Aidha, Waziri ameendelea kuwahimiza wanawake wajawazito kuhudhuria kliniki mapema kama ambavyo wataalamu wa afya wanashauri kuhudhuria mahudhurio manne kwa kipindi cha ujauzito wao ili kujua maendeleo ya ujauzito.

Send this to a friend