Karani atakayeshindwa kuzifikia kaya zote kutolipwa posho

0
24

Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imesema haitowalipa posho makarani watakaoshindwa kuzifikia kaya 150 kwa maeneo ya mijini na kaya 100 kwa maeneo ya vijijini.

Hayo yameelezwa na Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dkt. Albina Chuwa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Agosti 26 Jijini Dodoma.

”Karani yeyote ambaye hatokuwa amemaliza kuhesabu watu wake na hajafikia kaya 100 mpaka 150 kwa maeneo ya mijini kama Dar es salaam, tutaendelea kushikilia ile posho yake ya mwisho ambayo tulisema tutaitoa wakati akiwa amekamilisha zile kaya 150,” amesema Dkt. Chuwa.

Karani atakayepoteza kishkwambi kukatwa kwenye malipo yake

Aidha, Dkt. Chuwa ameongeza kuwa karani ambaye atakuwa na idadi ya kaya chache chini ya hizo zilizopangwa, atalazimika kwenda eneo lingine ili kukamilisha idadi hiyo.

Kuhusu mwenendo wa zoezi la utekelezaji wa Sensa, ameeleza kuwa zoezi hilo limefikia asilimia 54.

Send this to a friend