Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imezitaka klabu zote kuacha mara moja kufanya vitendo vinavyoashiria imani za kishirikina viwanjani.
Kamati imeeleza kuwa vitendo hivyo vinachafua taswira ya Ligi Kuu ya NBC, ambayo imejizolea umaarufu mkubwa barani Afrika.
Kocha wa Taifa Stars aondolewa
“Kuonesha vitendo hivyo hadharani ni kutangaza sifa mbaya, jambo ambalo linaweza kushusha hadhi ya Ligi hiyo, hivyo Kamati imepanga kutoa adhabu ya juu kwa klabu yoyote itakayofanya vitendo hivyo kuanzia tarehe ya taarifa hii,” imeandika TPLB.
Kwa mujibu wa kanuni ya 47:30, timu ikifanya kitendo chochote kinachoashiria imani za kishirikina, itatozwa faini ya kati ya TZS milioni 1 na TZS milioni 10.