Kulala kupita kiasi kunavyoweza kusababisha kifo

0
37

Kulala kupita kiasi kunaitwa hypersomnia au “kulala kwa muda mrefu.” Hali hii huathiri takribani asilimia 2 ya watu. Watu walio na hypersomnia wanaweza kuhitaji kati ya saa 10 hadi 12 za usingizi kila usiku ili kujisikia vizuri zaidi.

Kwa mujibu wa tovuti ya afya ya Healthline, ikiwa hupati usingizi wa kutosha mara kwa mara, mwili wako unaweza kujaribu kujirekebisha kwa kulala kupita kiasi. Pia watu wanaolala kwa muda mrefu wanaweza kuhisi uchovu kupita kiasi wakati wa mchana.

Kuna hali kadhaa za kiafya ambazo zinaweza kukufanya ulale kupita kiasi, kama vile masuala ya tezi, ugonjwa wa moyo, huzuni na aina fulani ya dawa.

Kwa watu walio na hypersomnia, kulala kupita kiasi kunaweza kusababisha
Wasiwasi, na matatizo ya kumbukumbu. Na wale wanaopendelea kulala muda mrefu hata kama hawana matatizo ya usingizi inaweza kusababisha pia athari mbaya kwa afya.

Baadhi ya matatizo hayo yanaweza kujumuisha maumivu ya kichwa, fetma, kisukari, maumivu ya mgongo, huzuni, ugonjwa wa moyo na kuongezeka kwa hatari ya kifo. Pia watu wanaolala kupita kiasi wanaweza kuwa katika hatari kubwa ya kupata ajali za magari.

Utafiti: Kulala saa chache chanzo cha watu kuwa wabinafsi

Hii ni miongozo ya muda gani unapaswa kulala kwa mujibu wa ‘National Sleep Foundation’ ya nchini Marekani;

Watoto waliozaliwa (0 hadi miezi 3): Saa 14 hadi 17

Watoto wachanga (miezi 4 hadi 12): Saa 12 hadi 15

Watoto wadogo (mwaka 1 hadi miaka 4): Saa 11 hadi 14

Watoto wa shule za awali: Saa 10 hadi 13

Watoto wa umri wa shule: Saa 9 hadi 11

Vijana: Saa 8 hadi 10

Watu wazima: Saa 7 hadi 9

Wazee: Saa 7 hadi 8

Send this to a friend