Morocco: Wanawake kupewa likizo yenye malipo wakati wa hedhi

0
28

Kikundi cha haki za kijami cha shirika la Bunge la nchini Morocco kimependekeza muswada utakaowaruhusu wanawake kupewa siku za likizo ya hedhi yenye malipo.

Pendekezo hilo linalenga kuboresha hali za wanawake kazini kupitia utoaji wa likizo ya hedhi yenye malipo ya siku mbili, ambapo wafanyakazi wa kike hawatahitajika kutoa ushahidi wa matibabu kila wakati wanapohitaji kuwa nyumbani.

Sheria 6 za usalama wa mwili unazopaswa kumfundisha mtoto wako

Aidha, limeeleza kuwa hedhi ni mwiko ndani ya jamii, hivyo kundi hilo linalenga kufungua mjadala kuhusu njia za kuondoa vikwazo vyote vinavyowakabili wanawake katika umma.

Endapo sheria hiyo itapitishwa na Serikali ya Morocco itakuwa nchi ya pili barani Afrika baada ya Zambia, ambayo ilipitisha sheria hiyo mwaka 2015 ikiwaruhusu wanawake kuchukua mapumziko katika kipindi chao cha hedhi.

Send this to a friend