Watoto wafariki baada ya wazazi kuwapaka kinyesi kukausha vitovu

0
23

Watoto takribani 306 katika Halmashauri ya Manispaa ya Kahama wamepoteza maisha kutokana na wazazi wao kuwapaka kinyesi cha wanyama kwenye vitovu vyao ili vikauke haraka.

Amebainisha hayo Mratibu wa Afya ya Uzazi wa mama na Mtoto Wilaya ya Kahama, Caroline Marcel wakati akizungumza na vyombo vya habari ambapo amesema watoto hao wamefariki katika kipindi cha Januari hadi Desemba, 2021.

Marcel amesema baadhi ya wazazi wamebuni mbinu mpya ya kutibu vitovu vya watoto wao wachanga kwa kuweka poda na kinyesi cha wanyama, jambo ambalo limekuwa likisababisha kupoteza maisha.

Ameongeza kuwa wanaendelea kutoa elimu ya afya ya uzazi ili kupambana na jambo hilo.

Chanzo: Nipashe