Miaka 80 kwa kosa la ubakaji

0
56

Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limewakamata watuhumiwa wawili ambao ni Paul Hilonga (60) mkazi wa Karatu kwa kosa la ubakaji, na Erasto Sias (24) mkazi wa Qurus Wilaya ya karatu kwa kosa la kubaka mtoto mwenye umri wa miaka 08.

Akithibitisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao, Kamanda wa Polisi mkoani humo, Kamishna Msaidizi wa Polisi, ACP Justine Masejo amesema Hilonga amehukumiwa kifungo cha miaka 50, huku Erasto akihukumiwa kifungo cha miaka 30 jela.

Mbali na hayo, Kamanda Masejo amesema amekutana na kuzungumza na askari katika Wilaya ya Karatu, na kubainisha kuwa kuna baadhi ya askari wanakwenda kinyume na maadili ya Jeshi la Polisi, hivyo Jeshi halitosita kuchukua hatua kwa askari wasiozingatia nidhamu, haki, weledi na uadilifu.

“Lazima tukubali ukweli huu kwamba kuna baadhi yetu bado tunakwenda kinyume na maadili mema ya Jeshi la Polisi. Nitoe wito kwa askari pamoja na wananchi, wakiona jambo lolote ambalo si sahihi, ni vyema watoe taarifa kwa viongozi wetu ili tuweze kuchukua hatua stahiki,” amesema Masejo.

Send this to a friend