Serikali yatangaza mlipuko ugonjwa wa Surua. Hizi ni halmashauri zilizoathirika

0
28

Serikali kupitia Wizara ya Afya imetangaza mlipuko wa ugonjwa wa surua katika Halmashauri saba nchini huku watu 38 wakithibitika kuwa na ugonjwa huo.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma Septemba 15, 2022 ambapo amesema wahisiwa walichukuliwa sampuli na kuzipeleka Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii kwa ajili ya uchunguzi.

Waziri Mwalimu amezitaja Halmashauri hizo kuwa ni Bukoba yenye sampuli tatu, Wilaya ya Handeni sampuli nne, Kilindi sampuli tatu, Mkuranga sampuli nne, Kigamboni nane, Manispaa ya Temeke 12 na Manispaa ya Ilala nne.

Aidha, ametoa rai kwa wananchi hususani wazazi na walezi kupeleka watoto chini ya miaka mitano kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ili wapatiwe chanjo ya Surua na Rubella, pamoja na kuwapeleka kwenye vituo vya afya wanapoona dalili za homa, mafua na vipele.

Send this to a friend