Serikali yaja na mkakati kuwezesha wanafunzi wote kupata chakula shuleni

0
26

Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imesema ili kupata matokeo mazuri ya elimu ni lazima kuhakikisha upatikanaji wa lishe bora shuleni ili kuwajengea wanafunzi afya bora na kupata utulivu wa akili wawapo madarasani.

Akizungumza Jijini Dodoma wakati wa hafla fupi ya utiaji saini fomu ya kujiunga na Muungano wa Chakula Shuleni, Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga amesema pamoja na kuwepo kwa sera hiyo, utoaji wa huduma ya chakula shuleni umekuwa ukitekelezwa katika shule kwa namna na viwango tofauti.

Amesema katika kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji, upatikanaji wa matokeo mazuri ya elimu hutegemea afya aliyonayo mwanafunzi huku sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 ikifafanua upatikanaji wa huduma muhimu katika shule na vyuo ikiwemo huduma ya chakula bora, maji safi na salama na upatikanaji wa huduma za afya kwa wanafunzi.

RC Makalla awaonya wanaosababisha hofu mitandaoni kuhusu panya road

“Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 inafafanua kuhusu upatikanaji wa huduma muhimu katika shule na vyuo ikiwemo huduma ya chakula bora, maji safi na salama na upatikanaji wa huduma za afya kwa wanafunzi ndio maana leo kwa pamoja hapa tunatia saini fomu ya kujiunga na Muungano wa Chakula Shuleni, nia ni ile ile ya kuhakikisha wanafunzi wanasoma vizuri na kupata matokeo mazuri . “amesema Kipanga .

Kipanga amebainisha kuwa mwezi Oktoba, 2021 Wizara ya Elimu ilizindua Mwongozo wa Kitaifa wa Utoaji wa Huduma ya Chakula na Lishe kwa Wanafunzi wa Elimumsingi ili kuweka utaratibu wa kitaifa ambao utawezesha wanafunzi kupata huduma hiyo muhimu.

Send this to a friend