Mwanamke jela miaka 30 kwa kusafirisha bangi kilo 13

0
26

Hadija Chilumba mkazi wa Tandika, Dar es Salaam amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela baada ya kutiwa hatiani kwa kusafirisha dawa za kulevya aina ya bangi kilo 13. 7.

Inadaiwa kuwa Chilumba alikuwa akisafirisha dawa hizo kutoka Lindi kwenda Dar es Salaam na ndipo alipokamatwa na polisi baada ya kufanya ukaguzi na kumkuta na majani ya bangi katika mabegi yake mawili Februari 27, mwaka huu katika eneo la Sido Manispaa ya Lindi.

Tahadhari kwa wanawake wanaotumia dawa za kusimamisha matiti

Mtuhumiwa aliiomba mahakama impunguzie adhabu hiyo kwa kuwa ana mtoto mdogo anayemtegemea mwenye umri wa miaka minne (4) pamoja na kusumbuliwa na maradhi mbalimbali ya mwili.

Hata hivyo, upande wa Jamhuri waliomba mahakama impe adhabu kali mtuhumiwa huyo ili ikawe fundisho kwa watu wengine kwa kuwa kilo 13.7 endapo zingefika kwa jamii basi nguvu kazi ya taifa ingepotea.

Send this to a friend