Serikali kuandaa ramani mpya ya Tanzania

0
95

Serikali kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imesema ina mpango wa kuandaa ramani mpya nchi nzima zinazoonesha sura ya nchi Tanzania Bara.

Naibu Waziri, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Ridhiwani Kikwete amesema bungeni Dodoma kuwa sura ya nchi huandaliwa ili kuonesha hali halisi iliyopo ardhini ikijumuisha taarifa za kijiografia za asili ambazo ni pamoja na mito, maziwa, milima na bahari, na zisizo za asili zinazojumuisha barabara, reli, mabwawa na miji.

Ameongeza kuwa moja ya sababu ya kuhuisha ramani ni kuonesha uhalisia wa sura ya nchi na kuhakikisha kuwa mabadiliko yanayotokea katika ardhi yanaoneshwa kwenye ramani mpya.

Aidha, amesema ramani hiyo itaandaliwa kupitia mradi wa kuimarisha miundombinu ya upimaji na ramani utakaotekelezwa kwa mkopo utakaotolewa na Serikali ya Korea kwa muda wa miaka minne kuanzia 2022/23 hadi 2025/2026.

Send this to a friend