DAWASA yatangaza Kukosekana kwa maji Septemba 23

0
16

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (DAWASA) imetoa taarifa ya kuzimwa kwa mtambo wa kuzalisha Maji, Ruvu chini ljumaa Septemba 23, 2022 kuanzia saa 12 asubuhi mpaka saa 2 usiku ili kuruhusu matengenezo ya bomba kuu maeneo ya Mlalakuwa na Mwenge.

Kwa mujibu wa DAWASA, maeneo yatakayoathirika ni pamoja na Bagamoyo, Zinga, Kerege, Mapinga, Mabwepande, Bunju, Tegeta,Mbweni, Boko, Salasala, Goba, Mivumoni, Kawe, Lugalo, Makongo, Chuo Kikuu, Mwenge na Kijitonyama.

Maeneo mengine ni Mikocheni, Msasani, Oysterbay, Masaaki, Mwananyamala, Kinondoni, Hospitali ya Taifa Muhimbili, Magomeni, Kigogo, Chang’ombe, Keko, Kurasini, Kigamboni, Airport, Kiwalani, Buguruni, Kigamboni, Vingunguti, Ilala na Katikati ya Mji.

Wakazi wa maeneo hayo wameshauriwa kuhifadhi maji ya kutosha wakati wa matengenezo.

Send this to a friend