Atakayebadilisha, kufichua taarifa binafsi faini milioni 10

0
27

Katika udhibiti wa ufichuaji taarifa binafsi sheria inayopendekezwa inaeleza kuwa mtu ambaye atabainika kuharibu, kufuta, kupotosha, kuficha au kubadilisha taarifa binafsi kinyume cha sheria atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi 100,000 na isiyozidi shilingi milioni 10 au kifungo kisichozidi miaka mitano au vyote kwa pamoja.

Masharti hayo ni sehemu ya mapendekezo ya Serikali katika Muswada wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi wa mwaka 2022, uliosomwa kwa mara ya kwanza bungeni Dodoma na Katibu wa Bunge, Nenelwa Mwihambi katika mkutano wa nane (8) wa bunge la 12 Septemba 23, 2022.

Baada ya miaka 43 madarakani, Rais wa Equatorial Guinea kugombea tena

Aidha, mtu atakayeuza taarifa binafsi ambayo imepatikana kwa ukiukwaji wa kifungu kidogo cha (1) anatenda kosa, hivyo adhabu yake ni kulipa faini isiyopungua shilingi100,000 na isiyozidi shilingi milioni 20 au kifungo kisichozidi miaka 10 au vyote kwa pamoja. Na ikiwa ni kampuni au shirika litalipa faini isiyopungua shilingi milioni 1 na isiyozidi shilingi bilioni 5.

Kwa mujibu wa sheria hiyo mkusanyaji ambaye bila sababu ya msingi atafichua taarifa binafsi kwa njia yoyote ambayo haiendani na madhumuni ambayo taarifa hiyo imekusanywa, anatenda kosa.

Send this to a friend