Orodha ya majina ya wanafunzi 640 waliokidhi vigezo vya Samia Scholarship

0
36

[pdf-embedder url=”https://swahilitimes.co.tz/wp-content/uploads/2022/09/SAMIA_SCHOLARSHIPS_PDF_FINAL.pdf”]

Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imefungua dirisha la maombi ya Samia Scholarship kwa wanafunzi 640 waliopata ufaulu wa juu kwenye masomo ya sayansi katika mitihani ya kidato cha Sita 2022.

Akitoa tangazo hilo Waziri wa Elimu, Prof Adolf Mkenda amesema wanafunzi hao ambao ni wa tahasusi za sayansi ambazo ni PCB, PCM, PGM, CBG, CBA, PMC na CBN, watafadhiliwa kwa asilimia 100 kwa kipindi cha miaka mitatu hadi mitano kulingana na programu husika walizodahiliwa.

Ameongeza kuwa ufadhili huo utazingatia viwango na miongozo ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kwa kugharamia ada ya mafunzo, posho ya chakula na malazi, vitabu na viandikwa, mahitaji maalum ya vitivo, mafunzo kwa vitendo, utafiti, vifaa saidizi kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum na bima ya Afya.

Wanafunzi hao wataanza kuomba ufadhili huo kuanzia kesho Septemba 28, 2022 kupitia tovuti ya Bodi ya Mikopo ya Mikopo kwa siku 14.

Aidha, Waziri Mkenda ametaja masharti saba ya ufadhili huo ikiwemo kiwango cha ufaulu wa mnufaika kisiwe chini ya GPA 3.8 katika mwaka wa masomo na chini ya hapo ufadhili utasitishwa.

Send this to a friend