Serikali imetoa masharti kwa wanafunzi 640 waliomaliza kidato cha sita wenye ufaulu wa juu katika masomo ya sayansi na hisabati wanaotarajiwa kupata ufadhili kupitia ‘Samia Scholarship.’
Haya ni masharti 6 yaliyotajwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda.
1. Mwanafunzi anapaswa kusoma, kuelewa na kusaini mkataba wa makubaliano ya ufadhili wa masomo kati yake na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
2. Anapaswa kuwa na akaunti ya benki kwa ajili ya fedha atakazolipwa moja kwa moja.
3. Mnufaika hatoruhusiwa kubadilisha programu ya masomo aliyopatiwa ufadhili bila barua ya idhini ya maandishi kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
Orodha ya majina ya wanafunzi 640 waliokidhi vigezo Samia Scholarship
4. Mnufaika hatoruhusiwa kuhairisha masomo isipokuwa kwa sababu za kiafya na kuthibitishwa na chuo husika.
Ikiwa mnufaika ataghairi fursa ya ufadhili kabla ya kuanza masomo, atapaswa kuwasilisha taarifa ya maandishi na kwenda kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
5. Iwapo kiwango cha ufaulu cha mnufaika wakati akiwa chuo kitashuka chini ya GPA 3.8 katika mwaka wa masomo, ufadhili utasitishwa.
6. Mnufaika anapaswa kujisajili katika mfumo wa Usimamizi wa Wananfunzi (Student Management System) unaopatikana katika tovuti ya wizara.