Historia yaandikwa Mtwara upasuaji wa kibingwa wa mifupa

0
44
  •  Upasuaji wa kibingwa wafanyika Mtwara kwa mara ya kwanza
  • Usimikaji wa mitambo ya kisasa umefanyika kwenye hospitali.

Huduma za kibingwa za Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) zimeanza kutolewa katika hospitali mpya na ya kisasa ya Rufaa ya Kanda Kusini Mtwara ambapo kwa mara ya kwanza historia imeandikwa kwa mgonjwa wa kwanza kufanyiwa upasuaji katika hospitali hiyo.

Zanzibar: Asilimia 27.4 ya vijana hawana ajira

Upasuaji huo wa kibingwa wa mifupa umefanywa na jopo la madaktari bingwa, wauguzi na wataalam wa usingizi kutoka MOI kwa kushirikiana na wataalamu wa hospitali hiyo.

Kiongozi wa jopo la wataalamu kutoka MOI, Dkt. Albert Ulimali amesema jopo la wataalam 11 limepiga kambi ya siku tano kutoa huduma za kibingwa za mifupa, ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu ikiwa ni pamoja na kuwafanyia upasuaji wagonjwa.

Dkt. Ulimali amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu (MB) kwa ujenzi wa hospitali Kanda Kusini pamoja na usimikaji wa vifaa vya kisasa.

Send this to a friend