Alama nyekundu ni onyo ambalo hukuonesha tatizo katika uhusiano uliouanzisha.
Ikiwa kuna viashiria vya kutisha vinavyonekana awali zaidi ya mara moja katika uhusiano wako, ni muhimu kuzingatia kabla ya uhusiano kwenda mbali sana.
Hivi ni viashiria 9 ambavyo hupaswi kuvipuuza;
Hakupi nafasi: Anataka tu kuwa na wewe, ingawa hilo linaweza kusikika kuwa jambo la kupendeza, lakini anajaribu kukuhimiza kukata uhusiano wako kwa marafiki na familia.
Hufanya kazi kila wakati: Kazi yake inachukua nafasi ya kwanza zaidi ya wakati wenu pamoja, na wala hasiti kughairi tarehe au kukuacha ili kuhudhuria kile ambacho ni muhimu zaidi kwake.
Mbinafsi: Mipango unayopanga naye inahusisha tu kile anachokitaka yeye kufanya, na kila mara mawazo yake ndiyo sahihi. Mara nyingi anachukia usipofanya baadhi ya vitu kwake, lakini kwake ni kawida kutovifanya vitu hivyo kwako.
Anakubadilisha: Hujaribu kukubadilisha kila wakati kwa njia anayotaka yeye ilimradi ufanye kila anachokitaka.
Marafiki/ ndugu zako hawapendezwi naye: Familia yako na marafiki zako hawamuoni kama ni mtu sahihi kwako.
Mchunguzi: Hutaka kuangalia jumbe zako binafsi au kutaka kujua kila kitu chako binafsi, na kama utamkatalia kufanya hivyo hujawa na hasira na kukutuhumu kwa kuwa mkaidi kwake.
Mambo yako sio muhimu kwake: Hajivunii mafanikio yako na wala hashiriki katika mafanikio yako.
Hatendi haki: Sio mtu wa haki, anapenda kukutawala kimwili au kihisia.
Unamuepuka: Unakaa kimya na kubeba tabia yake chafu kwa sababu kukabiliana naye mara kwa mara kunakuchosha.