Wazazi wawakata watoto kinyama cha ulimi ili wawahi kuongea

0
51

• Wazazi wanawakata watoto wao kinyama kilichopo chini ya ulimi ili wawahi kuongea.
• Daktari wa Kinywa na Meno amesema uvumi huo unasababishwa na waganga wa tiba za asili.

Baadhi ya wazazi katika Manispaa ya Kahama wanawakata watoto wao kinyama kilichopo chini ya ulimi (uvula) kwa imani ya kuwa kukiondoa husaidia watoto wao kuongea mapema.

Inadaiwa mtoto wa umri wa miaka minne alipoteza maisha baada ya wazazi wake kumkata kinyama kinachoitwa kitaalamu uvula (wengine hukiita uzi) ili kusaidia mtoto kuongea na kupakwa kinyesi cha ng’ombe kilichosababisha shingo kuvimba na kupoteza maisha.

Mwanamke ahukumiwa kifungo cha maisha kwa kubaka mtoto

Mama mzazi wa mtoto huyo, Sabrina Hamis mkazi wa Nyasubi Manispaa ya Kahama amekiri kumpeleka mtoto wake kwenye tiba za asili na kutoa TZS 80,000 ili mtoto wake aondolewa kinyama hicho.

Daktari wa Kinywa na Meno kutoka Hospitali ya Manispaa ya Kahama, Athumani Juma amesema uvula ni kiungo kilichopo kwenye taya la juu na kazi yake ni kuzuia maji au chakula kisiingie puani, na pia ni kiungo kama kiungo kingine kwenye mwili. Hivyo kukawia kuongea kwa mtoto hakuhusiani na kiungo hicho.

“Huu uvumi umesababishwa na waganga wa tiba asili kutokana na wazazi kutoona watoto wao wachanga wakitoa sauti wakati wa kulia au wenye umri kuanzia miezi sita hadi miaka mitano wakichelewa kuongea.” amesema.

Send this to a friend