Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) umeweka wazi kuwa kwa sasa imejipanga kuongeza mabasi mengine 177 kutokana na yaliyopo kutotosheleza mahitaji ya usafiri ya umma.
Mkurugenzi Mtendaji wa DART, Dkt. Edwin Mhede wakati wa kikao cha pamoja baina ya viongozi wa taasisi hiyo, wakuu wa wilaya na wakuu wa polisi katika wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam, amesema wakati wowote DART itasaini mkataba na mzabuni kisha mabasi hayo yatawasili nchini ndani ya kipindi cha miezi sita.
“Usanifu wa mradi wa mwendokasi wakati unaanza makadirio yalikuwa mabasi 305 na sasa tubayo mabasi 210. Yaliyopo hayatoshelezi mahitaji, ndiyo sababu tunatarajia kuongeza mengine 117 hivi karibuni,” amesema.
Aidha, amesema kutokana na mahitaji ya watu, DART iliamua kupeleka huduma hiyo kutoka Muhimbili hadi Mlongazila ili watu wanaougua au kuuguza wafike kwenye hospitali hizo kwa urahisi.