Kunyimana tendo la ndoa chanzo kikubwa cha migogoro ya familia

0
43

• Wanandoa kunyimana tendo la ndoa ni chanzo cha migogoro, msongo wa mawazo na ukatili  dhidi ya watoto.

• Kesi nyingi zinazoripotiwa katika dawati la jinsia, chanzo ni kunyimana tendo la ndoa.

Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Muze, Sumbawanga mkoani Rukwa, Valentine James amesema tabia ya baadhi ya wanandoa kunyimana tendo la ndoa ni miongoni mwa sababu zinazochochea migogoro, msongo wa mawazo na ukatili dhidi ya watoto.

Amesema katika dawati la jinsia liliko kituoni hapo, migogoro mingi iliyoripotiwa na wanandoa inatokana na kunyimana tendo la ndoa na kusababisha hasira baina yao hivyo kupelekea watoto kuathirika zaidi.

“Mwanandoa anapokuwa na hasira na akashindwa kumwadhibu mwezi wake, anahamishia hasira zake kwa watoto, hivyo wamekuwa wakipigwa na kuumizwa, chanzo chake ni hasira za mzazi kutokana na mgogoro wa ndoa pamoja na msongo wa mawazo,” amesema.

Ang’atwa ulimi na mpenzi wake wakijamiiana usiku

Aidha, amebainisha changamoto nyingine ni baadhi ya wanaume kuwa na tabia ya kuchukua mazao ya chakula nyumbani na kwenda kuyauza kisha kufanya starehe na wanawake wengine hali inayosababisha kuibuka kwa migogoro ndani ya familia.

Send this to a friend