Fabian Sebastian, mkazi wa Ubungo jijini Dar es Salaam amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa kosa la kuwadhalilisha marais wastaafu wa Tanzania.
Wakili wa Serikali, Grace Mwanga alidai Sebastian anashtakiwa kwa makosa mawili ambayo ni kuwadhalilisha Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi na awamu ya nne, Jakaya Kikwete kupitia mtandao wa Tik Tok.
Makonda na Lemutuz washtakiwa kwa tuhuma za kupora Range Rover
Amesema Septemba 21, 2022 mshatakiwa kupitia akaunti yake ambayo inafahamika kama fabylee, katika maeneo yasiyojulikana aliweka picha za marais hao wastaafu na kuweka ujumbe wa kuwadhalilisha .
Kwa upande wa mshitakiwa alikana mashitaka hayo huku hakimu akimtaka mshitakiwa kuwa na wadhamini wawili wenye barua za utambulisho ambao wanapaswa kuwa wakazi wa Dar es Salaam.