Sababu 5 kwanini wanaume na wanawake hupeana talaka

0
27

Kuna sababu nyingi kwa nini ndoa huvunjika na kuishia kupeana talaka, lakini baadhi ni sababu za kawaida ambazo huathiri mahusiano. Daktari na mkufunzi wa maisha Dkt. Chandni Tugnait anaelezea kwa nini wanandoa wanaamua kutengana.

1.Mawasiliano

Mawasiliano duni kati ya wanandoa ni sababu ya ndoa nyingi kuvunjika. Inaweza kuwa vigumu kuendelea kuwa pamoja  ikiwa hakuna mawasiliano mazuri na ikiwa huwezi kuwasiliana katika mazingira ya wazi na ya uaminifu na mpenzi wako kuhusu mahitaji na matakwa yako.

2. Kukosa uaminifu

Uaminifu unapovunjika inaweza kuwa vigumu sana kurekebisha. Ikiwa umedanganywa, unaweza kupata shida kumwamini mwenzako tena. Na hata ikiwa unaweza kusamehe na kuendelea na uhusiano, uamimifu uliojengwa hauwezi kuwa kama hapo awali.

3. Matatizo ya kifedha

Matatizo ya pesa mara nyingi hutajwa kuwa sababu kuu ya kupeana talaka. Pengine wewe na mwenzi wako mnabishana kuhusu pesa, hamna malengo sawa ya kifedha au mapenzi hupungua pindi pesa inapokuwa adimu, inaweza kuwa vigumu kukaa pamoja na kudumu kwa muda mrefu.

4. Kukosa ukaribu

Ukaribu sio tu kuhusu kujamiina. Inahusu uhusiano, mapenzi, na kuwa karibu na mwenza wako. Ikiwa hamna ukaribu pengine ni kutokana na kujali zaidi au umbali uliopo kati yenu,  inaweza kusababisha hisia za upweke na chuki na baada ya muda inaweza kuathiri hata uhusiano.

5. Ugomvi

Kwa bahati mbaya, unyanyasaji wa nyumbani ni sababu ya ndoa nyingi kuishia kwenye talaka. Ikiwa wenzi hawaelewani na kufikia hatua mbaya zaidi ya kupigana mara kwa mara, uhusiano mara nyingi huishia kuvunjika.

Send this to a friend